Jahazi (Swahili Poem)

Maji, nisogezee jahazi kwangu

Mimi Abiria, nilie potea

Nakuvutwa mikononi mwako

Mafichoni naogelea,

Nakuzama, tena sana.

Huvutwa kwa zana

zilizo baridi

Ni nini unacho kitafuta kwangu

Mimi mwana, nilie potea

Nakutokea mikononi mwako

Mikono yanao ni kaba.

Ni wapi univutapo

Maana sifaham mahali hapa

Mkono wako unirudishe,

Kwa familia, salama

Na kwa jahazi iliyo potea.

Niruhusu nijitoe kwako

Nipumue upepo nilicho zoea

Nipigwe na jua

na kukauka

Tukutane tena siku ya mvua

Comments 3
Loading...